Simba Wa Mziki,
- ADDO MUSIC
- Oct 18, 2021
- 3 min read
Updated: Oct 19, 2021
Kenya kunao Simba wa muziki.simba hawa,wana uwezo mkubwa katika mabadiliko ya muziki na biashara ya muziki hapa nchini Kenya na bara nzima la Afrika.
Jogoo wa shamba kweli hawiki mjini.Lakini katika ulimwengu wa wa mziki,hilo ni tofauti.
Hapa nchini Kenya kunao simba wa mziki wanaotawala ndani na nje ya mbuga zao.
Mziki wa kizazi kipya humu nchini,umevamiwa na kila kijana wa kike na wakiume.
Kutokana na ushindani mkali wa kila mmoja kutaka kuonekana bingwa katika fani hii ya mziki, baadhi ya wanamziki wameanza kujikweza kileleni katika chati za muziki na majina yao kushamira.
Nachosema ni kuwa,katika kila shughuli muhimu anayojihusisha mwanadamu, lazima pawepo na uongozi.
Katika tasnia hii muhimu,hapa nchini Kenya,simba wa muziki wameweza kujitokeza ili kuongoza wengine.
Simba hao wa muziki ndio nani?
Otile Brown
Otile Brown,ndiye Simba wa muziki kwa sasa hapa nchini Kenya.
Otile,ni mtunzi wa haiba ya juu wa muziki.
Muziki wake,huwateka mashambiki wake kutokana na mpangilio mtulivu wa vina,mdundo,ujumbe na sauti yake pamba.
Muziki wa bwana umejawa na hisia tele na kupambwa na lugha safi ya mahaba.
Ngoma za Otile Brown zinapendwa sana humu nchini kwa sababu zimetulia na kupangika.
Kwa sasa hivi,Otile anatawala chati za muziki hapa nchini na kuwa na wasajili wengi (subscribed)katika akaunti yake ya Youtube.
Anajumla ya 930k subscribers juu kuliko msanii yeyote nchini Kenya.
Ngoma zake kufikia sasa zina jumla ya wat
azamaji milioni 191M.
Kevin Bahati
Bahati (Mtoto wa MaMa),ni msanii wa pili wa muziki hapa nchini Kenya kuwa na subscribers wengi katika akaunti yake ya You tube.Bahati anajimla ya 799K.
Ngoma za bahati zimetazamwa na watu milioni 133M.
Bahati ni msanii ambaye amejituma sana kimuziki.
Willy Paul
Willy Paul(Bwana Mkunaji)
Ni msanii ambaye hupenda sana kiki na mara nyingi mashabiki huwa hamuelewi.
Willy Ponze,ameweza kutajwa katika sikendo nyingi zinazompa sifa mbaya.
Msanii huyu hutumia sikendo ili kusukuma kazi zake.
Willy Paul,ndiye msanii wa tatu Kenya kuwa na idadi kubwa ya subscribers katika akaunti yake ya You tube.
Anajumla ya 797K.
Ngoma zake zimeweza kutazamwa na watu milioni 151M.
Willy Paul ndiye mbingwa wa kiki hapa nchini Kenya.
Hivi maajuzi,amehusishwa na kisa cha kumdhulumu kimapenzi Miss P.
Sauti Soul
Sauti Soul,ni kundi la wanamuziki wanne Bien, Polycarp,
Kundi hili lina ushawishi mkubwa katika bara la Afrika.Sauti Soul wameweza kushinda tuzo kadhaa ikiwemo Afrima.
Sauti Soul ni wasanii wa nne kuwa na ufuasi mkubwa katika akaunti ya You tube.wana subscribers 796K.
Ngoma zao zinaongoza kuwa na idadi kubwa ya watazamaji wapatao milioni 203M.
Kundi hili limeweza kutawala chati za muziki nchini Kenya kwa mitindo yao ya Afro Music unaowavutia wengi kama kibao chao cha Susana.
Sauti Soul wanaweka bayana umuhimu wa kutia bidii maishani.
Khaligraph Jone
Papa Jones,ni msanii wa kifoka yaani wa rap hapa nchini Kenya.
Anatambulika sana katika mtindo wake wa kufoka kwa kasi.
Anatambulika kwa kina la OG.
Khaligraph Jones anasubscribers 500K
katika akaunti yake ya mtandao wa You tube.
Ngoma zake zimetazamwa mara milioni 61M.
Nyashinski
Nyashinski,ndiye anayetufungua ukurasa wa sita bora katika muziki wetu wa hapa nchini Kenya.
Nyashinski ana subscribers 435K.
Ngoma zake katika mtandao wa you tube,zimetazamwa na watu milioni 83M.
Msanii huyu anazidi kujituma kila kukicha.
Je,nani ndiye Simba wa kike kimziki nchini Kenya?
Nadia Mukami
Nadia Mukami ndiye malkia wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Kenya.
Nadia ni msanii mwenye bidii ya kuigwa mfano.
Tangu aingie katika fani hii ya muziki, Nadia uachia vibao kila mwaka, mwezi,wiki na siku.
Ngoma zake zinachezwa sana humu nchini.
Nadia ana youtube subscribers 402K.
Ngoma zina idadi ya watazamaji milioni 49M.
Jamani,wacheni Kanadia katambe.
Femi One
Utawezana?Femi One ni mwanadada ambaye kazi yake na Mejja utawezana,ilimfungulia mlango mkubwa wa kutambulika.
Femi One ana youtube subscribers wapatao 219K.
Mwanamuziki huyu hajui chochote kuhusu kukata tamaa.
Vivian
Vivian,ni mwanamuziki aliyejaliwa na sauti ya kipekee.Ngoma zake ni kivutio cha wengi hapa nchini Kenya.
Vivian,anajumla ya you tube subscribers102K.
Vivian ni mrembo wa sura na sauti pia.
Jovial
Kikweli, Jovial ni msanii ambaye ana mtindo wake kitofauti.Sauti yake imepambwa na utamu unaotekenya masikio na kupenya moyoni.
Msanii huyu huwa mara nyingi wanapotoa ngoma na Otile Brown,wimbo huo unakuwa mtamu na wakuvutia.
Jovial ana 66K youtube subscribers.
Nikita Keling
Ni msanii ambaye anajulikana kwa kibao chake kinachoitwa Ex.
Umaarufu wake umejulikana sana tangu aachie wimbo huo.Ameweza kuteuliwa katika tuzo za AFRIMA mwaka huu.
Anajumla ya 115K
Subscribers katika akaunti yake ya You tube.
Nikita,ni mwanga wa Kenya kimataifa.
Ana uwezo wa kupeperusha bendera yetu ya Kenya kimataifa kupitia fani hii ya mziki.
Wahu Kagwi
Wahu alianza safari yake ya mziki kitambo kidogo na bado hajawahi vua uwanamuziki ndani yake.Wahuana ushawishi mkubwa kwa vijana wa leo ambao wapo katika tasnia hii ya mziki.
Wahu ana subscribers 92.9K
katika akaunti yake ya You tube.
Sanaipei Tande
Ni mwanamuziki na muigizaji tajika hapa nchini Kenya.
Sanaipei,anawavutia vijana wengi sana katika ulingo huu wa sanaa.
Sanaipei Tande amefanya ushirikiano ama collabo na wasanii tajika humu nchini kama vile,Jua Cali,Otile Brown,Nadia Mukami.
Sanaipei ni muigizaji katika kipindi cha Kina katika Maisha Magic.
Avril
Tukiwataja Simba wa muziki,hatuwezi msahau Avril.Amekuwa kutoka kitambo hadi sasa anatamba.
Muziki kweli hulipa na kulisha ukiufanya na nidhamu.@Mc Lion Simba
+254 703810704.





































Comments